RAPA maarufu nchini Afrika Kusini, Cassper Nyovest ameshinda pambano la ngumi aliloandaa kati yake na shabiki ambaye amekuwa akimkosoa na kumkosea heshima mara nyingi rapa huyo mitandaoni.


Nyovest alitumia muda mfupi kumpiga shabiki huyo Slik Talk ulingoni katika pambano hilo lililopewa jina la "Fame and Clout."

Shabiki huyo ambaye ni mwandaaji wa maudhui kupitia YouTube na amekuwa akitumia mtandao huo kumponda Nyovest, alilipwa TZS milioni 14 kwa kukubali pambano na kuahidiwa kiwango kama hicho endapo angeshinda.

Nyovest amekuwa akitajwa kuwa ni miongoni mwa wasanii wasiopendwa kuchafuliwa majina yao wala kusemwa vibaya.