Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya RB Leipzig Christopher Nkunku atakosa fainali za kombe la dunia nchini Qatar baada ya kuumia mazoezini akiwa na timu ya taifa.
Nkunku amepata majeraha amepata majeraha ya Mguu kufuatia kuchezewa Tackling mbaya na kiungo wa Real Madrid Camavinga ameumia siku nne kabla ya kuanza rasmi kwa fainali hizo Jumapili Novemba 20, 2022.
Kikosi cha Kocha Didier Deschamps tayari kinamajeruhi kadhaa ambao watazikosa fainali hizo akiwemo Kiungo wa Chelsea N'Golo Kante na kiungo wa Juventus Paul Pogba.
Mabingwa watetezi Ufaransa itafungua dimba dhidi ya Austaralia Jumanne Novemba 22.

0 Maoni