Klabu ya Chelsea imeshindwa kumudu kununua mafuta ya mabasi yake kutokana na akaunti za benki za klabu hiyo kufungwa na Serikali ya England.



Hali ya kiuchumi ya klabu hiyo kubwa duniani ni mbaya mno baada ya Serikali ya Uingereza kuweka kizuizini mali za mmiliki wake, Roman Abramovich; raia wa Urusi ambaye anadaiwa kusapoti nchi yake hiyo kuivamia Ukraine.

Hali inaonekana kuwa tete zaidi huku baadhi ya wadhamini wengine wakijiandaa kuacha kuidhamini klabu hiyo.