Habari njema kwa mashabiki Simba wapo katika harakati za kumrudisha kiungo mkabaji Gerson Fraga raia wa Brazil kwa ajili ya kuziba pengo la kiungo Taddeo Lwanga ambaye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara Lwanga ameshindwa kuitumikia Simba.



“Lwanga ana tatizo kubwa ambalo linahitaji upasuaji utakaomuweka nje kwa muda mrefu jambo ambalo timu itahitaji kupata mbadala wake kwa kuwa inakabiliwa na mashindano makubwa ya kimataifa na kuhitaji kuutetea ubingwa wa ligi kuu msimu huu ,” 


Simba inahitaji kiungo mkabaji ili kuja kuongeza nguvu  Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Kiungo kutoka Mali Sadio Kanuote.