Pambano la kuwania ubingwa wa IBF kati ya  bondia Selemani Kidunda katika raundi ya tatu limesababisha kumalizwa bila mshindi (kwa sare) dhidi ya bondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Tshimanga Katompa usiku wa kuamkia leo, baada ya Kindunda kupata jeraha juu ya jicho

Kidunda alichanika juu ya paji lake la uso baada ya kugongwa na kichwa cha Katompa jambo lililomsababishia kushindwa kuendelea na pambano hilo kutokana na kuvuja damu nyingi kwasababu ya jeraha kuwa kubwa.


Kwamujibu wa msimamizi wa mkanda huo ni kuwa bondia Selemani Kidunda angeweza kupewa ushindi endapo pambano hilo lingefika raundi ya nne kwani jeraha alilolipata lilitokana na kuchezewa mchezo usio wa kiungwana kwa makusudi na mpinzani wake aliyetumia kichwa kumjeruhi lakini sheria za IBF zinawalazimu kutoa matokeo ya sare kwasababu tu tatizo hilo limejitokeza katika raundi ya tatu.