Cameroon itafungua pazia la michuano ya mataifa huru Afrika AFCON dhidi ya Burkina Faso, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Olembe uliopo mji wa Yaounde ambao ndiyo mkubwa katika mashindano hayo ukichukua watazamaji 60,000.
Michuano hii ilikuwa inasubiriwa kwa hamu baada ya mwaka jana kushindwa kufanyika kutokana na janga la corona ambalo bado linaendelea kuitikisa dunia kwa sasa. Hakika yatakuwa mashindano yenye mvuto, kutokana na kusheheni mastaa kibao kutoka kona mbalimbali za ndani na nje ya Afrika.
Bingwa mtetezi Algeria
anapewa nafasi ya kutetea ubingwa huo wakiongozwa na nyota wa Manchester City
Riyad Mahrez.
Senegal wakiwa na Sadio Mane Misri chini ya Mohamed Salah bila Pamoja na mwenyeji Cameroon wanapewa nafasi ya kutwaa ubingwa huo, Mali watakuwa na Staa wa Liverpool Sadio Kanute
0 Maoni