Ofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF Jacqueline Kamwamu amemshataki Polisi Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez, mashtaka hayo yamefunguliwa katika kituo Kikuu Cha Polisi Jijini Dar es Salaam.
Siku ya Alhamisi ya Januari 20 Barbara alipokea wito wa kufika kituoni hapo ambapo baada ya kufika aliwekwa ndani kwa saa nane kisha kusomewa shtaka lake.
Akizungumza na mtangazaji
wa kituo cha Redio cha Efm Maulid
Kitenge leo Januari 24 , Barbara amesema hii ni vita ya nje ya uwanja ambayo
klabu ya Simba inapitia.
"Hii vita inaonekana
ni kubwa zaidi, na Unajua ukubwa na uzito wa vita ambayo Simba imeipata lakini
tutaendelea kupambana, na vita sio Uwanjani tu kuna vita nyingine nje ya Uwanja
ambayo imenishika pabaya"
Shtaka linalomkabili Barbara ni kutoa lugha isiyopendeza kwa Afisa wa TFF Jacqueline Kamwamu ambae alimzuia asiingie uwanjani katika eneo la VIP na Watoto wadogo siku ya Desemba 11, 2021 katika mchezo kati ya Yanga na Simba ambao uliisha kwa sare ya 0-0
0 Maoni