Mabingwa
Watetezi wa Afcon Algeria jana walianza kutetea ubingwa wa michuano hiyo kwa
suluhu dhidi ya Sierra Leone mchezo wa kundi E.
Tofauti
na matarajio ya wengi Algeria imeshindwa na kuondoka na alama tatu baada ya
Sierra Leone kuonyesha moyo wa kujituma na kuizua safu ya Ushambuliaji
ikiongozwa na Riyad Mahrez anayechezea Manchester City ya England na Yacine
Brahimi.
Shujaa
wa mchezo huo alikuwa mlinda mlango wa Sierra Leone Mohamed
Kamara ambaye aikuwa mchezji bora wa mechi hiyo akizuia michomo
mingi na kuiweka timu yake salama.
Mohammed Kamara wa Sierra Leone alifanya aliokoa michomo saba katika mechi dhidi ya Algeria, na kuweka rekodi ya golikipa aliyefanya saves nyingi zaidi katika AFCON bila ya kuruhusu goli tangu Ovono wa Equatorial Guinea afanye hivyo katika mechi dhidi ya DR Congo mwaka 2015.
Suluhu hiyo inaifanya Algeria kufikisha mechi 35 bila
kufungwa wakiifukuzi rekodi ya mabingwa wa ulaya Italia ya michezo 37 bila
kufungwa.
0 Maoni