Bingwa mtetezi wa AFCON Algeria rasmi leo Januari 20, imeutema ubingwa huo baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Ivory Coast, kipigo hicho kinawafanya kumaliza nafasi ya mwisho kwenye kundi E wakiwa na pointi 1.

 



Magoli ya Ivory Coast yamefungwa na Frank Kessie dakika ya 22’ Ibrahim Sangare 39 na goli la tatu limefungwa na mchezaji machachari wa Arsenal Nikolas Pepe dakika ya 54’

 

Goli pekee la Algeria limefungwa Sofiane Bendebeka dakika ya 73’ Ivory imefuzu kwa hatua ya mtoano baada ya kujikusanyia alama 7 na Equtorial Guinea imamaliza nafasi ya pili ikiwa pointi 6 na kufuzu kwa hatua ya mtoano.

 


Algeria kwenye michuano ya msimu imetolewa ikiwa haijafanikiwa kuonja ushindi, ikitoka sare mbili na kufungwa mechi moja.