Klabu ya Watford imemtimua Meneja wake Claudio Ranieri , miezi mitatu baada ya kuteuliwa kuwa Meneja wa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya England.
Ranieri ambaye aliteuliwa Octoba mwaka jana ametimuliwa baada ya kupoteza michezo saba kati ya nane ya mwisho aliyocheza kwenye EPL.
Watford ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo wakiwa na point 14 kwenye michezo 20 waliyocheza hadi sasa.
Muitaliano huyo aliipa ubingwa wa ligi kuu Leicester City msimu wa mwaka 2015/ 16
0 Maoni