Klabu ya Arsenal inajiandaa kumpa mkataba mpya wa miaka miwili meneja wa timu hiyo Mikael Arteta ili  kuendelea kuinoa timu hiyo baada ya bodi ya the gunners kuridhika  na uwezo alionyesha tangu achukue mikoba ya Unai Emery miaka miwili iliyopita.

 


Mabosi  wa Arsenal wamefurahia mpango wa  Arteta kuwatumia vijana zaidi kwenye kikosi hicho pamoja usimamizi mzuri wa nidhamu kwa wachezaji wenye majina makubwa.  

 

Mkataba wa sasa wa Arteta unaisha mwakani 2023, na kumekuwa na tetesi kuwa Manchester City wanamuona kama mtu sahihi wa kumridhi Pep Guardiola ambaye huenda akaondoka City baada ya mkataba wake kuisha mwakani.