Arsenal  imevutiwa na kiungo wa Leicester City, Youri Tielemans, na imeshaanza mazungumzo na mawakala wake juu ya uwezekano wa kumsajili.

 


 Mikel Arteta anataka kuboresha safu yake ya kiungo baada ya kumruhusu Ainsley Maitland-Niles kwenda Roma kwa mkopo.

 

Kwa mujibu wad  Daily Mail, Arsenal wameshaanza mazungumzo ya kumnasa Mbelgiji huyo, 24, ambaye amebakiza miezi 18 kwenye mkataba wake na Leicester.