Australia, kwa mara ya pili imesitisha kibali cha kuingia
Nchini humo cha Mchezaji maarufu wa Tenesi, Novak Djokovic kutokana na utata
kuhusu kukaa Nchini humo bila kuchoma chanjo ya Covid 19.
Uamuzi huu uliotangazwa na Waziri wa masuala ya Uhamiaji wa
Australia, Alex Hawke ambaye amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuzingatia sheria ya afya ya taifa hilo hatua inayomaanisha ana uwezo wa kumfukuza
Mchezaji huyo.
Licha ya uamuzi huu, Djokovic bado ana uwezo wa kufungua
jalada jingine la kesi kupinga kufukuzwa Nchini humo.
Djokovic ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo ya Australia Open
0 Maoni