Leo usiku saa
2:15 itapigwa fainali ya kombe la Mapinduzi 2022 kati ya Azam Fc dhidi ya
Mnyama Simba kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Azam wamingia
fainali baada ya kuwatoa mabingwa watetezi Yanga kwa mikwaju ya penati 9-8
baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu, huku Simba ikiitungua Namungo Fc kwa magoli
2-0.
Historia inaonyesha
hii itakuwa fainali ya Nne, tatu zilizopita wana lamba lamba Azam fc wameibuka
washindi na kuondoka na kombe.
Je leo Azam
ataendeleza ubabe mbele ya Simba? Au Mnyama atafuta uteja na kuibuka na ushindi
tusuburi dakika 90 zitaamua.
0 Maoni