Bao pekee la Nahodha, beki mkongwe Aggrey Morris dakika ya 30 lilitosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Transit Camp katika mchezo wa hatua ya 32 ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) mchezo ulipigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana , januari 28,
Kwa ushindi huo, Azam FC inakwenda hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ya (ASFC), ambako itamenyana na timu ya daraja la Kwanza, Bagamoyo Friends iliyoitoa Catamine jana.
Mechi nyingine za jana za Azam Sports Federation Cup, Namungo FC imeitoa Lindi United kwa kuichapa 2-0 uwanja wa Ilulu mjini Lindi na Pamba FC imeitoa Stand United kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
0 Maoni