Baada ya kuizuia safu ya
ushambuliaji ya Simba kushindwa kupata bao hapo jana Januari 22, beki wa Mtibwa Sugar Abdi Banda amesema
kuwa washambuliaji hao mabingwa ni laini na wamecheza bila kuwapa usumbufu.
“Unajua mastraika wa Simba ni mastraika ambao ni laini sana mechi ya leo nimecheza kwa ku- relax kuliko hata ya KMC unapokutana na mafowadi wanaosubiri kupewa mipira inakuwa rahisi kwa difenda kucheza"
"Bocco, Kagere, Mugalu wote wanasuburi kupewa
mipira ingekuwa changamoto kama wanakimbia huku na huku maana hakuna difenda ambaye anaruka kwenda hewani kuliko mimi.”
Jana Mtibwa Sugar, ilifanikiwa
kuondoka na alama moja baaa ya kutoka sare ya 0-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya
NBC uliochezwa kwenye uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro..
0 Maoni