Huenda huu ukawa msimu mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa
Barcelona baada ya jana Januari 20, kutolewa kwenye hatua ya 16 bora ya Copa de
Rey dhidi ya Athletic Club baada ya kuchezea kichapo cha mabao 3-2.
Iker Muniain alikuwa
wa kwanza kutikisa nyavu za Barcelona mapema tu dakika ya 2’ Barca wakasawazisha
kupitia kijana waliyemsajili kutoka Manchester City, Ferran Torres dakika ya 20.
Inigo Martnize akaipa uongozi Athleti Club dakika ya 86,
vijana wa Xavi Hernandez wakarudi mchezonu baada ya Pedri kusawazisha na
kufanya matokeo kuwa 2-2 dakika 90+3, Muniain kwa mara nyingine akaipa ushindi
Athletic kwa bao la Mkwaju wa Penati kwenye dakika 30 za nyongeza (Etra Time)
Msimu huu Barcelona wameondolewa kwenye Copa del Rey raundi 16 kwa kufungwa 3-2 na Athletic Bilbao, Wametolewa hatua ya makundi Uefa Champions
League na sasa wanashiriki Ueropa League, wameondolewa kwenye nusu fainal ya Super Cup na mahasimu wao
wakubwa Real Madrid na sasa wapo nafasi
ya 6 kwenye msimamo wa La Liga.
0 Maoni