Beki wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda amewaomba radhi wadau wa soka
nchini Tanzania kufuatia kauli za kejeli
alizotoa dhidi ya wachezaji wa Simba alitoa kauli hizo baada ya mchezo wa ligi kuu uliopigwa Manungu
Complex Jumamosi (Januari 22) na kuisha kwa sare 0-0
Beki huyo ambaye amewahi
kucheza soka Afrika Kusini kabla ya kurejea nchini msimu huu, kupitia ukurasa
wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika
“Tuanze wiki mpya yaliyopita si ndwele tugange yajayo Huenda
niliwaudhi au kuwakera wengi kila mmoja kwa nafasi yake naomba mnisamehe sana”
“Kwenye mpira au kwenye mchezo wowote kuna maneno ya kejeli na
dharau kwa mpinzani wako au hata mchezaji mwenzako lakini hamaanishi kuna
uhasama kama wengi walivyopokea maneno yangu, michezo ni furaha na ajira basi
tusichukulie kila kitu personal/serious sana'”
“Naomba mnisamehe sana maana kila mtu ana upokeaji wake na
tafsiri yake, sikuwa na lengo la kumbagua Henock Inonga au wachezaji wengine wa
Simba tusahau yaliyopita, tupo kwa ajili
ya kujenga na kuutangaza mpira wetu na sio chuki wala ubaguzi wowote hasa kwa
wachezaji wanaokuja kucheza hapa kwetu”
0 Maoni