Nyota wa Real Madrid Karim Benzema amefunga bao lake la 300 Real Madrid wakati Real iliposhinda
4-1
dhidi ya Valencia juzi kwenye La Liga.
Benzema ambaye
alifunga mabao mawili dakika ya 43 na 88, bao lake la pili lilikuwa la 300
kwake katika mechi 584 kwenye misimu yake 13 Real Madrid. Sasa ni mfungaji bora
namba nne nyuma ya Alfredo de Stefano (308), Raul (323), na kinara Cristiano
Ronaldo (450)
“Tulikuwa na wakati mgumu katika michezo yetu miwili ya
kwanza kutokana na namna ambavyo wapinzani wetu walikuwa wakikamia na kufanya
matumizi makubwa ya nguvu. “Kwa kuwa hakuna muda mrefu wa kupumzika, hivyo
tutalazimika kufanya mabadiliko kadhaa ya kikosi kutokana na namna ambavyo
mahitaji ya kikosi chetu yalivyo, na utimamu wa wachezaji husikia.
0 Maoni