Majogoo wa jiji Liverpool, wamefanikiwa na kuibuka na
ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brentford
kwenye mchezo wa ligi kuu ya England uliopigwa leo katika dimba la Anfield.
Liverpool kwa mara ya kwanza wamecheza bila ya Mohamed Salah, Sadio Mane ambao wapo
kwenye majukumu ya timu za taifa kwenye michuano ya Afcon inayoendelea Cameroon.
Magoli ya Fabinho, Alex Oxlade-Chamberlain Takumi
Minamino yalitosha kuipa alama tatu muhimu Liverpool na kuweka hai matumaini ya
kuifukuzia vinara wa ligi hiyo Manchester City.
Liverpool imefikisha alama 45 alama 11 nyuma ya City
wenye alama 56,ambao wamecheza mechi moja zaidi ya Liverpool.
0 Maoni