BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko machache kwenye ratiba ya Ligi Na ya NBC yakiathiri tarehe za michezo 12, muda wa kuanza kwa michezo sita na kuipangia tarehe michezo mitatu ambayo haikuwa na tarehe kwenye ratiba ya awali pamoja na rmchezo wa kiporo kati ya Kagera Sugar na Simba SC.
Mabadiliko hayo yamelenga kuepuka uwepo wa michezo ya viporo kutokana na ushiriki wa Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) huku michezo mitatu ikipangiwa tarehe baada ya kufaharnika kwa hatma ya ushiriki wa klabu nne (Yanga, Simba, Azam na Namungo) katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.
Ratiba ya awali ya Ligi Kuu ya NBC ilizingatia ushiriki wa klabu nne (Sirnba, Yanga, Azam na Biashara United) kwenye michuano ya CAF kwa kuzipatia nafasi ya kutosha kwa ajili ya maandalizi, safari na kucheza mechi za michuano hiyo nyumbani na ugenini.
0 Maoni