Bodi ya ligi kuu Tanzania TPLB imeufungia uwanja wa mabatini Uliopo Mlandizi mkoani Pwani kuendelea kutumika kwenye michezo ya ligi kuu hadi hapo utakapofanyiwa marekebisho kwenye eneo la kuchezea (Pitch)

 


Eneo la uwanja linatakiwa kusawazishwa vizuri na majani yake kustawishwa vema ila kuendana na matakwa ya kikanuni na sheria namba ya mpira wa miguu inayozungumzia uwanja

 

Klabu ya Ruvu Shooting ambayo ilikuwa ikitumia uwanja huu kama uwanja wa nyumbani italazimika kutumia uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam.