Klabu ya Barcelona inawinda Saini ya kiungo mshambuliaji wa
Manchester United Bruno Fernandes iwapo watashindwa kumpata kinda wa Erling
Haaland.
Tangu alivyofunga hat-trick dhidi ya Wolves mwanzoni mwa
msimu huu kiwango Fernandes kimekuwa cha
kushuka nakupanda akifunga magoli mawili tu kwenye michezo 16.
Mapema wiki hii Rais wa Barca Joan
Laporta alikaririwa akisema wanajuandaa kuishangaza dunia kwani wanataka
kushusha wachezaji wakubwa kwenye dirisha la usajili.
Staa huyo wa Ureno amekuwa mchezaji muhimu kwa United kwa
misimu miwili amefunga magoli 45 asisti 34 kwenye michezo 105
Tangu kuwasili kwa Cristiano Ronaldo Bruno ameshuka kiwango
akifunga magoli 5 kwenye michezo 18 ya Epl.
0 Maoni