Wenyeji wa Afcon Cameroon imetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Afcon baada ya
kushinda kwa mbinde dhidi ya Comoro waliokuwa pungufu kwa kuifunga mabao 2-1 mchezo ulipigwa jana Usiku
Mapema dakika
ya 7’ nahodha wa Comoro Jimmy Abdou alitolewa kwa kuoneyeshwa kadi nyekundu,
dakika ya 29’ Karl Toko Ekambi akawainua wenyeji na kuipa uongozi Cameroon.
Mfungaji bora
mpaka sasa Vicent Abobakar aliingia kambani kwa mara nyingine tena dakika ya 70’
Abobakar anaongoza kwa ufungaji akwa na magoli 6 na asisti 1.
Comoro ambao
walionyesha moyo wa kupambana walifnikiwa kupata bao kupitia kwa Youssouf
M'Changama aliyepiga faulo ya viwango na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Comoro
wameingia kwenye mchezo huo bila ya wachezaji wengi muhimu baada yakuibanika
kuwa na Covid-19 akiwemo kipa wao tegemeo na kipa mwingine kuwa
majeruhi hivyo kuwalazimu mchezaji wa ndani kwenda kudaka.
Cameroon sasa itakutana na Gambia ambao waliwaduza Guinea kwa kuifunga bao 1-0 na kuandika historia ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki Afcon na wametinga hatua ya robo Fainali itakayochezwa Januari 29.
0 Maoni