Staa Zambia wa Klabu ya Simba, Clatous Chota Chama, amewasili nchini jioni na hii ya leo Januari 14, 2022  na kutambulishwa rasmi kujiunga tena na mabingwa hao wapya wa Mapinduzi Cup na Mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi Kuu ya Nbc.


 


Triple C amejiunga na Simba akitokea Rs Berkane ya Morocco kwa mkataba wa miaka miwili na amewakili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwao Zambia.


Chama aliondoka Simba Augusti 13,  2021 na kujiunga  na RS Berkane ya Morocco na sasa anarejea baada ya kudaiwa kushindwa kuzoea mazingira nchini Morocco.



 

Berkane imesema sababu kubwa ya Chama kuondoka Morocco ni kushindwa kuzoea mazingira ya nchi hiyo kwa haraka pamoja na masuala ya kifamilia.