Mabingwa wa Ulaya Chelsea, jana usiku Januari 18, wameshindwa
kufurukuta mbela ya Brighton & Hove Albion baada ya kulazimishwa sare ya
1-1 katika mchezo wa ligi kuu England uliochezwa katika dimba la Amex, England.
Vijana wa Thomas Tuchel walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu
kupitia Hakim Ziyech kipindi cha kwanza dakika ya 28' kabla ya Adam Webster's kuzawazisha kwa
kichwa dakika ya 60 kipindi cha pili
Sare hiyo imeifanya The
Blues kufikisha alama 44 na hivyo kuachwa
alama 12 na vinara wa ligi Manchester City wenye pointi 56.
0 Maoni