Chelsea
imetinga hatua ya fainali ya kombe la Carbao Cup baada ya ushindi wa bao 1-0
dhidi ya Tottenham Hotspur mchezo wa nusu fainali ya pili na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-0 mchezo
uliopigwa usiku wa kuamkia Januari 13.
Goli
pekee la The Blues limefungwa na mlinzi Antonio Rudiger dakika ya 18 ya mchezo kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona na kuipa
uhakika Chelsea kucheza fainali katika uwanja wa Wembely.
Chelsea
inasubiri mshindi kati ya Liverpool na Arsenal ambao wanashuka dimbani leo
Januari 13.
0 Maoni