Kocha wa Tottenham Hotspurs Antonio Conte jana usiku amekaribishwa kwa kipigo kwenye dimba la Stamford Bridge dhidi ya Chelsea, baada ya kukubali kichapo cha mabao  2-0 mchezo wa kombe la Carbao Cup mzunguko wa kwanza.



Magoli yote ya Chelsea yamepachikwa kipindi cha kwanza na   Mjerumani Kai Havertz na goli la pili lakujifunga la beki Ben Davies Kwenye  mchezo wa jana kocha Tomas Tuchel  alimuanzisha mshambuliaji Romelu Lukaku

 

Hatua hiyo imekuja  baada ya  Mbelgiji huyo kuomba radhi kutokana na maneno aliyotoa wiki iliyopita ambayo kuwa hana furaha na Maisha ndani ya Stamford Bridge na anatamani kurejea Inter Milan