Inaweza kushtua kidogo lakini ndio uhalisi kiungo mshambuliaji wa barcelona Philippe Coutinho amekubali kujiunga na aston villa kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu.





Kocha wa Villa Steven Gerrard ambaye alicheza na  Coutinho wakiwa Liverpool ndiye aliyemshawishi   kujiunga na Villa.

Villa wana Imani kuwa Coutinho ataisadia timun  hiyo sambamba na kurejesha makali ya kiungo huyo Fundi wa Ki- Brazil.

Vilabu kadhaa vya England vilikuwa vikiwinda kupata Saini ya Coutinho lakini ameamua kutimkia Villa kuungana na Gerrard.