Wasanii wakubwa Barani Afrika na duniani kutokea pande za Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun ‘Wizkid na David Adedeji Adeleke ‘Davido’ wamemaliza tofauti zao na sasa hivi wakikutana ni amani.



Hii imetokea Ijumaa usiku baada ya mastaa hao ambao wamekuwa mahasimu kwa muda mrefu kukutana club nchini Nigeria na kukumbatiana, jambo ambalo limeleta furaha kwa mashabiki wao kuona wakipatana tena.