Novak
Djokovic atatetea michuano ya wazi ya Australia *Austaralia
Open) 2022 licha ya kuwa hajapata chanjo
ya UVIKO-19 baada ya Mahakama ya Australia kuwa mchezaji namba moja kwa ubora
Duniani kwenye Tenisi, kuachiliwa huru na kwenda kushiriki michuano hiyo.
Hakimu
wa kesi hiyo amesema kuwa ameona kuwa hakuna madai yoyote ya msingi kufuatia
kuzuiliwa kwa hati ya kusafiria ya Djovo na Ofisa wa mpakani katika uwanja wa
ndege wa Melbourne.
Jaji Antony
Kelly ameamua hati ya kusafiria aliyokuwa anatumia Djokovic ni halali na
anaruhusiwa kuingia nchini Australia ilikuweza kuweza kushiriki mashindano ya
wazi ya Australia.
Mashindano ya
Australia Open yanatarajia kuanza Januari 17, ambapo Djokovic anaingia kwenye
michuano hiyo kama bingwa mtetezi akiwa ameshinda taji la Grand Slam mara tisa.
0 Maoni