Mcheza Tenisi Nambari Moja Duniani Novack Djokovic amezuiwa
kuingia Austaralia baada ya kugundulika visa yake kutokidhi vigezo vya kuingia kwenye taifa hilo.
Djokovic ambaye ni Bingwa Mtetezi wa Austalia Open, alishikiliwa
katika uwanja wa ndege wa jiji Melbourne, hilo kwa saa kadhaa kabla ya vikosi
vya mpakani kutangaza kuwa hajakidhi sheria za kuingia na atafukuzwa.
Katika
taarifa, Jeshi la Mpakani la Australia lilisema Djokovic "alishindwa kutoa
ushahidi ufaao ili kukidhi mahitaji ya kuingia Australia, na visa yake imefutwa.
Mwaka jana
Staa huyo wa Tenis alipinga chanjo hatua inayotajwa kuwa imechochea Sakata ka
kuzuiwa kuingia Austalia.
0 Maoni