Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Soka Tanzania Bara TPLB imemuondoa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu mwamuzi wa kati kutoka Tanga, Hance Mabena kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.




Hatua hiyo imekuja kwenye tukio la mchezaji wa Yanga Djuma Shabani kuchezewa rafu kabla hajalipiza kwa kupiga kiwiko.

 Mwamuzi msaidizi namba moja Paschak Joseph kutika Shinyanga na mwamuzi wa akiba Jackson Samwel kutoka Arusha wameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa kushindwa kumsaidia mwamuzi wa kati katika kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu kwenye tukio la mchezaji Djuma Shabani kuchezewa rafu kabla hajalipiza kwa kupiga kiwiko.