Legendi wa zamani wa Soka wa Camaeroon na Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo, Samuel Eto’o amesema kuwa Mataifa ya Afrika yanayo nafasi kubwa ya kushinda Kombe la Dunia kuliko Bara la Ulaya na Mabara mengine kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji awa Afrika wanaocheza huko Ulaya.
Eto’o amesema kinachoiangusha Afrika ni kudharauliana, kutopendana na kutopenda mafanikio ya wenyewe kwa wenyewe.
“Nachofahamu sisi Waafrika hatuna umoja na muungano. Tunadharauliana sisi kwa sisi. Nikwambie kitu Afrika tuna vipaji halisi kuliko Ulaya.
“Lakini kwanini hatushindi kombe la Dunia? Huwa inaniumiza sana hali iyo. Natamani nishuhudie nchi moja Afrika ikitwaa taji hilo kubwa Duniani.
0 Maoni