Klabu ya Everton ya England imemtimua
kazi kocha wake Rafael Benitez baada ya mfululizo wa matokeo yasioridhirisha kwenye mechi za ligi kuu ya Epl.
Benitez anaingia kwenye
historia ya klabu hiyo kwa kuwa kocha aliyefundisha muda mchache akichukua
timu hiyo mwezi Juni 2021 akidumu kwa miezi mitano tu, Rafa alichukua nafasi hiyo ambayo iliachwa wazi na Carlo Anchelotti aliyetimkia Real
Madrid.
Mchezaji wa zamani wa
timu hiyo aliyewika na Manchester United, Wayne Rooney anapewa nafasi ya
kuchukua mikoba ya Benitez.
0 Maoni