Kufuatia matokeo mabaya ya timu ya Taifa Ghana katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea, Wizara ya michezo ya nchi hiyo katika mkutano wa dharura siku ya Ijumaa iliagiza Chama cha Soka cha Ghana kumfukuza kazi kocha wake Mserbia, Milovan Rajevac.
Rajevac kwa kipindi chake cha kwanza akiwa na Black Stars aliiongoza Ghana kutinga fainali za AFCON 2010 na Robo fainali ya Kombe la Dunia la 2010.
Alirejea Septemba 2021 katika awamu yake ya pili hakikwenda kama ilivyotarajiwa kwani Ghana walitoka AFCON 2021 bila kupata ushindi, na kuandika mpya kwa Black Stars.
0 Maoni