Timu ya Taifa ya Ghana maarufu Black Stars imetupwa nje ya muchuano ya Afcon jana usiku baada ya kufungwa mabao 3-2 na Comoro katika mchezo wa kundi C.

 


Ghana ililazimika kucheza pungufu baada ya Nahodha wao Andrew Ayew kutolewa kwa kadi nyekundu dakika 25 ya mchezo.

 

Pamoja na kucheza pungufu Ghana ilionyesha kiwango bora tangu kuanza kwa mashindano hayo, mpaka dakika ya 64 walikuwa nyuma kwa magoli mawili na wakafanikiwa kuzawazisha magoli hayo ndani ya dakika 8 kupitia kwa Richmond Boakye dakika ya 64 na Alecnder Djiku dakika ya 77.

 

Kwa upande wa Comoro magoli yao yalifungwa na El Fardou Mohamed mapema kabisa dakika ya 4’ na Ahmed Mogni aliyeweka wavuni magoli mawili 61’ 85’.

 

Katika kundi C Morocco na Gabon zimefuzu kwa hatua ya mtoano