Mchezaji wa Manchester United Mason Greenwood amekamatwa kwa tuhuma za ubakaji na shambulio kufuatia madai  video kwenye mitandao ya kijamii.



 

Polisi wa Greater Manchester walisema ilifahamishwa kuhusu “picha na video za mitandao ya kijamii zilizotumwa na mwanamke akiripoti matukio ya unyansaji wa kingono”.


 

 “tunaweza kuthibitisha kuwa mwanamume mwenye umri wa miaka 20 amekamatwa kwa tuhuma za ubakaji na shambulio”.

 

Kinda huyo anaendelea kuzuiliwa kwa mahojiano na uchunguzi unaendelea, Klabu ya Manchester United hapo awali ilisema mchezaji huyo hatarejea kwenye mazoezi au mechi hadi pale polisi watakapothibitisha tuhuma hizo.


Nyota huyo anatuhumiwa kumshusjia kipigo  kumuumiza vibaya mpenzi wake anayefahamika kama Harriet Robson.