Nyota wa Manchester United Mason Greenwood amekumbwa na kashfa ya kumshambulia na kumuumiza vibaya mpenzi wake anayefahamika kama Harriet Robson.



Harriet ambaye pia ni mwanamitindo ametumia mtandao wake wa Instagram kuweka video ikionyesha akiwa na majeraha mbalimbali sehemu za usoni na miguuni na kuwajulisha wafuasi wake kuwa aliyefanya hivyo ni mpenzi wake Mason Greenwood.


Klabu ya Manchester United imetoa taarifa ikieleza kuwa inafuatilia kwa ukaribu tuhuma hizo zinazosambaa kwa kasi mitandaoni ili kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua zaidi