Meneja wa Manchester City Pepe Guardiola, pamoja na msaidizi wake Juanma Lillo wamekutwa na maambukuzi ya Corona na watakosekana kwenye mchezo wa raundi ya tatu kombe la Fa Swindon Town kesho Ijumaa.

 


Wafanyakazi 21 wa Manchester City wapo Karantini baada ya kugundulika kuwa na virusi vya ugonjwa huo.

 

Shurikisho la soka la England FA bado haijatoa tamko kuhusu mchezo huo kama utachezwa au kuahirishwa, michezo kadhaa imepigwa kalenda kutokana timu janga hilo.

 

Kocha msaidizi Rodolfo Borrell anatarajiwa kuingoza City dhidi ya Swindon Town kwenye mchezo huo wa Fa.