Kocha wa timu ya taifa ya Italia, Roberto Mancini amumjumuisha mshambuliaji Mario Baloteli ikiwa imepita zaidi ya miaka mitatu, tangu mtukutu huyo kuitwa kwenye kikosi hicho.

 




Baloteli 31, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Adana Demirspor hajachezea timu ya taifa tangu mwezi Septemba 2018.

 

Super Mario ameichezea Italia michezo 36 akichezea michuano ya Euro mwaka 2012 na kombe la dunia mwaka 2014 lillofanyika nchini Brazil.