Historia inaenda kuandikwa kwenye michuano ya
AFCON ambayo inaanza leo huko Cameroon, kwa Salima Mukansanga kuwa mwanamke wa
kwanza kuwa mwamuzi kwenye mashindano hayo makubwa barani Afrika.
Mwamuzi huyu kutoka Rwanda anakuwa miongoni mwa waamuzi wanne wa kike watakaosimamia mashindano hayo wakiwemo kutoka Cameroon Carine Atemzabong, Fatiha Jermoumi wa Morocco na Bouchra Karboubi ingawa wao hawatachezesha mechi.
Salima ni mzoefu na tayari amesimamia mechi kadhaa ikiwemo za Kombe la Dunia la Wanawake, Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake na Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF.
0 Maoni