Inter Milan imefanikiwa kutwaa taji la Supercopa Italian baada ya kuicharaza Juventus 2-1 usiku wa kuamkia leo Januari 13.




 

Juve ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 25 tu ya mchezo huo kupitia kwa Weston McKennie baada ya kupokea pasi kutoka kwa Alvaro Morata.


 

Dakika 10 baadaye Lautaro Martinez aliisawazishia Milan kwa mkwaju wa penati baada ya Mattia De Sciglio wa Juventus kumchezea rafu Edin Dzeko.


 

Mpaka dakika 90 zinamalizika, miamba  hiyo ya Italia  ilikuwa imetoshana nguvu ndipo zikaongezwa dakika nyingine 30.


 

Bao la dakika ya mwisho ya mchezo huo (dakika ya 120+1) lililofungwa na mshambuliaji kutoka Chile Alexis Sanchez baada ya kupokea assist ya Matteo Darmian lilitosha kuwapa Inter taji hilo na kuuanza vyema mwaka 2022.