Beki wa Timu ya Taifa ya Uganda Juuko Murshid ambaye aliwahi kukipiga na   mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Juuko Murshid ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ akiwa na umri wa miaka 27.



Juuko ametangaza kuachana na ‘The Cranes’ kupitia barua yake aliyoiwasilisha kwenye Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), na sasa ataendelea na jukumu moja tu, la kuitumikia klabu yake Express FC ya Uganda.


Katika Barua hiyo Juuko ameandika: “Nimeitumikia nchi vya kutosha na ni wakati wa mimi kupumzika


“Haukuwa uamuzi rahisi lakini pamoja na familia yangu na uongozi wangu, tumefikiri na kuona ni uwamuzi sahihi. Ninawashukuru FUFA, wachezaji wenzangu na wadau wote wakati nilipokuwa na Uganda Cranes.