Simba leo Januari 26, imepoteza mechi ya pili msimu huu kwenye ligi ya NBC, baada ya kukubali
kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar, mchezo uliochezwa uwanja wa Kaitaba
Bukoba mkoani, Kagera.
Goli la wakata miwa wa Kagera limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba Hamis Kiiza dakika 71 chache baada ya kuingia.
Katika mchezo Kiiza alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonekana
anapoteza muda na awali tayari alikuwa na kadi ya njano.
Licha ya Kocha Pablo kuanza na bila mshambuliaji asilia lakini wachezaji walishindwa kutumia nafasi waliozotengeneza
Pengo la pointi limesalia kuwa 10 baina yake na vinara wa ligi watani zao wa jadi Yanga wanaoongoza wakiwa na alama 35 huku Simba akiwa na 25.
0 Maoni