Kwa Mujibu wa Daily Mail nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo, atakatwa asilimia 25 ya mshahara
wake endapo Manchester United, ikishindwa kumaliza nafasi ya nne za juu kwenye msimamo wa ligi na hivyo
kukosa fursa ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya (Uefa Champions
League).
Ronaldo amefunga magoli 14 katika mechi 23 tangu arejee United, kwa sasa anapokea
mshahara wa paundi laki 385,000 kwa wiki utashuka mpaka paundi laki 288,000
United ipo ya nafasi saba, pointi mbili nyuma kuifikia West Ham United
lakini wapinzani wengine wa Top Four Arsenal na Totenham Hotspur wamecheza
mechi pungufu.
Ronaldo alikubali kupunguza mshahara wa paundi 500,000 kwa
wiki kutoka Juventus ya Italia lakini bado anabaki kuwa mchezaji anayelipwa
mkwanja mrefu akifuatiwa na kipa David de Gea anayelipwa paundi laki 375,000
kwa wiki.
0 Maoni