Mlinda mlango wa Mtibwa Sugar, Jeremia Kisubi hatacheza mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Simba Sc kutokana na mkataba wake wa mkopo kutocheza mechi dhidi ya Simba.



Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amethibitisha hilo leo  Januari 19, alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Wasafi Fm.



Huenda  Shabani Kado akapewa  jukumu la kusimama kwenye milingoti mitatu naada ya mtibwa kumpoteza mlinda mlango Aboutwalib Msheri aliyejiunga na Yanga.