Mchezaji wa zamani wa Manchester United Andy Cole amesema kiwango cha  kiungo wa Manchester United Bruno Fernandes kimeshuka tangu ujio wa  mreno mwenzake Cristiano Ronaldo.






Cole amesema Bruno wa msimu huu si yule wa msimu uliopita ambaye alikuwa bora, msimu uliopita 2020/21 alifunga magoli 28, akiwa na asisti 17 kwenye mechi 58 huku akicheza mechi 37 kati ya 39 za ligi kuu ya England.

 

United ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha wa muda Ralf Rangnick ina shika nafasi ya 7 ikiwa na alama 31, kwenye msimamo wa EPL.