Imetimia miaka miwili sasa tangu Staaa wa Kikapu (Basketball) nhini Marekani  kutoweka kwenye uso wa dunia pamoja na mtoto wake, ambao walifariki kufuatia ajali ya Helikopta.



Ajali hiyo ilitokea Mwaka juzi (2020) 26 Januari, moja ya sababu zilizotajwa ni spidi kali juu ya anga kwa zaidi Maili 160 kwa lisaa kwenye anga chafu.

Mchongaji wa sanamu huko Los Angeles ameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Kobe na Gigi Bryant kwa kuweka sanamu ya wawili hao mahali ambapo waliagwa kwa huzuni mnamo 2020.


 Mchongaji wa sanamu hiyo, Dan Medina, ameiambia TMZ Sports kwamba aliunda umbo la shaba la pauni 160 na kulivuta hadi eneo la tukio huko Calabasas.