Klabu ya Yanga imekuwa na nafasi kubwa sana msimu huu wa kuweza kutwaa ubingwa wa NBC Premier League hali hii imeonekana baada ya klabu hiyo kuanza vizuri sana toka mwanzoni mwa msimu huu hadi sasa licha ya kuanza vizuri laikini pia wakiwa na wachezaji bora sana katika kikosi chao.
Yanga hadi sasa imecheza michezo 13 na kuvuna alama 35 na kupotenza alama 4 tu katika michezo yake ambapo wapinzani wao Simba Sc wakiwa wamecheza michezo 13 na kuvuna alama 25 huku wakiwa wamepoteza alama 14 kwa takwimu hizi Yanga wamekuwa na nafasi kubwa sana hadi sasa kuweza kutwaa ubingwa msimu huu wakiwa wanamuombea mpinzani wao aendelee kufanya vibaya katika mechi zake zijazo.
.
Wananchi kwa sasa ndio timu pekee inayoonekana kufanya vizuri sana ukilinganisha na timu zingine katika NBC premier League ambapo imekuwa na wachezaji wazuri sana na wakuelewana katika kila idara sio beki sio viungo sio washambuliaji wote wameonekana kupambana sana wakiwa uwanjani na kuweza kusaka alama tatu kwa pamoja ambapo hali hii inawafanya Yanga kuonekana kuwa bora sana katika msimu huu wa 2021- 2022.
Kunukia kwa ubingwa Yanga ni pamoja na wapinzani wao kuonekana kufanya vibaya sana katika michezo yao huku wakiendelea kuwa na matokeo mabaya ambapo wameweza kupoteza mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar bao 1-0 huko mkoani Kagera katika uwanja wa Kaitaba.
0 Maoni